Posts

Showing posts from July, 2018

HII NDIO THAMANI YA MWANAMKE.

Mwanamke ni kama Jua unaweza usione umuhimu wake, yaani kila siku unaenda mjini jua lipo tu, unaliangalia lakini huangalii umuhimu wake kwako. Wakati mwingine likiwa kali unaanza kulalamika kuwa linachoma na lina kera. Lakini ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila jua maisha yasingekuwepo. Chakula tunachokula ni kwasababu ya Jua, mvua ikinyesha sana mafuriko yakitokea tunatamani jua, kwenye baridi tunatamani pia jua, Hatuliwazii kwasababu lipo tu na linatimiza majukumu yake kimya kimya bila kelele. Hiyo ni sawa na mwanamke, ukishaoa kuna mambo ambayo mwanamke huyafanya na baada ya muda unaanza kuyaona ya kawaida kawaida, chakula kinakuwa mezani kila siku hujui kinapikwaje na vyombo vinaoshwaje, anabeba mimba na watoto wanazaliwa hujui maumivu aliyoyapata lakini unatabasmu na kucheka ukijisifia watoto wangu na hata mkigombana unasema niachie wanangu wewe nenda tu tafikili unajua maumivu aloyapata kipindi anawaleta duniani ao watoto. Watoto wanaumwa mpaka wanapona hujui hata wam